Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

KOZI YA UJASILIAMALI NA UBUNIFU KWA VIJANA KATIKA ULIMWENGU WA KIDIJITALI

UTANGULIZI

Ulimwengu  wa karne ya ishirini na moja ambazo ni zama za kidijitali kwa sehemu kubwa sana umeathiri kila eneo la maisha ya mwanadamu hasa vijana wakiwa ndio wahanga wakubwa. Mfumo wa ajira umebadirika sana, karne ya 21 si karne ya kujivunia tena taaluma au fani fulanni, karne ya 21 ni karne ya fursa. Hivyo vijana wanapaswa kuandaliwa kisaikolojia na kifikra ili waweze kuona fursa mbalimbali zilizoko katika mazingira yao.Kwa sehemu kubwa vijana wengi wana elimu ya taaluma Fulani lakini hiyo elimu yao haijwakomboa kifikra ili kuweza kupata maisha bora ya ndoto yao. Kwa bahati mbaya sana ulimwengu umebadirika lakini elimu wanayopewa vijana kuanzia ngazi ya msingi, sekondari, ufundi na vyuo haijabadirika.

Tafiti nyingi zinaonesha kuwa vijana na wanafunzi waliopata mafunzo ya ujuzi wa ujasiliamali wana mtazamo chanya kuhusu ujasiliamali. Hata hivyo kuanzisha sera madhubuti kwajili ya kuendeleza biashala ndogondogo itakuwa na tija tu pale ambapo vijana wa kike na wa kiume wako tayari na wamewezeshwa kupambana na changamoto za ujasiiamali. Ujasiliamali ni ubunifu inaanza na uwezo wa kifikra wa kijana kuweza kubuni, kupanga na kutekeleza wazo na kulibadirisha likawa kitu halisi. Ndoto bila mipango ya utekelezaji ni sawa na imani pasipo matendo. Kwa hivyo, ujuzi wa matumizi ya kompyuta na ujuzi wa biashara ya e-biashara zinalenga kuimarisha ubunifu kwa mtu binafsi ili kuwa na uhusiano na fursa za biashara za kimataifa na kupata faida.

Elimu ya ujasiliamali na matumizi sahihi ya vifaa vya komputa ni muhimu katika kuongeza ujuzi kuhusu biashara kwa vijana ili wale wanaoweza kuchagua wawe na nguvu ya kufanya maamuzi na hatua zinazo hitajika katika kubadilisha ndoto zao za kibiashara kuwa uhalisia.

LENGO LA MAFUNZO

Baada ya mafunzo washiriki watapata:

1: Ujuzi wa kuwasaidia kutengeneza utamaduni wa kifikra za kijasiliamali miongoni mwa vijana kama vile uwezo wakubuni  kuendeleza na kusimamia biashara/miradi

2: Kupata ujuzi utakao ongeza uwelewa wa fursa na changamoto za kijasiliamali na kujiajiri

3: kuwapa washiriki uelewa wa kina wa majukumu na mchango ambao vijana wanaweza kutoa ili kutengeneza maisha yao ya baadae na ya nchi kwa kuwa na ujuzi maeneo kazini na taaluma zao

4: kuendeleza mtazamo chanya kuhusu miradi endelevu, kujiajiri na ujasiliamali wa kijamii.

5: Kuwaandaa washiriki na ujuzi wa matumizi bora ya kompyuta na mbinu za vyombo vya habari vya kijamii ambazo zitasaidia kuvutia, na kujenga fursa ya biashara.

6: kuwandaa vijana kuwa wafanya kazi bora kwa kuongeza uelewa wa kina kuhusu usimamizi wa biashara na miradi.

WASHIRIKI WA MAFUNZO

Walimu, wakufunzi, wajasiliamali, wafanyabiashara, vijana, wazazi/walezi, viongozi ngazi ya serikali za mtaa na wanafunzi wa shule za msingi ,sekondali, vyuo vya ufundi, vyuo vikuu na walio maliza shule na vyuo.

Ukumbi:                DAR ES SALAAM

MUDA:  3 SIKU TATU KWA WIKI KUANZIA TAREHE : 25 FEBRUARI  HADI 15 MACHI 2019.

Mafunzo hayo yatafanyika siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kuanzia saa Nane Mchana.

Course Properties

Course date: 18-03-2019 2:00 pm
Course End Date: 05-04-2019 5:00 pm
Capacity Unlimited
Location Tanzania Global Learning Agency (TaGLA)
We are no longer accepting registration for this event