Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Mbali na Mafunzo na Huduma za Mikutano kwa Njia ya Video, TaGLA inatoa huduma mbalimbali za ushauri. Baadhi ya huduma za ushauri zinazotolewa na TaGLA ni;

  • Kuratibu na Kusimamia Shughuli mbalimbali
  • Ukaguzi wa kumbi za Mikutano kwa Njia ya Mtandao
  • Kuweka mipangilio ya Mikutano kwa Njia ya Mtandao
  • Kuandaa Makabrasha
  • Kutoa Mafunzo Maalum kama Yanavyoombwa

TaGLA inatoa mafunzo ya kozi mbalimbali, unaweza kuangalia kozi ambazo tunatoa ama program za mtandaoni, mafunzo ya ana kwa ana (AKA), Midahalo ya Kimataifa au hata Mikutano kwa Njia ya Video. Wawezeshaji wetu wenye ujuzi mkubwa na uzoefu wa kutosha pamoja na vifaa tulivyo navyo vinatuwezesha kutoa huduma bora ndani na nje ya nchi.

 

UkiwaTaGLA utapata vifaa anuwai vya mawasiliano kiteknolojia ikiwa ni pamoja na projekta, compyuta zilizounganishwa kwenye mkongo wa mawasiliano ya Intaneti. Kuna maabara mbili za vifaa anuwai vya mawasiliano, moja ina kompyuta 30 (Chumba cha Kilimanjaro cha Vifaa vya Mawasiliano ya Kiteknolojia) na nyingine ina kompyuta 18 (Chumba cha Mikumi cha Vifaa vya Mawasiliano ya Kiteknolojia). Hata hivyo, tuna kompyuta pakatwa (laptops) ambazo zinaweza kuunganishwa popote kwenye vyumba vyetu na kwenye maeneo ya wateja wetu pale inapohitajika.

Teknolojia ya Mikutano kwa Njia ya Video husaidia kuendesha mikutano miwili au zaidi kwa wakati mmoja na huwawezesha washiriki kuwasiliana kupitia video na kusikia sauti.TaGLA, ambayo inaongoza nchini Tanzania kwa kutoa huduma za mikutano kwa njia ya video, tuna uzoefu wa zaidi ya miaka kumi na tano (15) na tuna wataalamu wa kutosha katika uwanja huu, na hivyo tanafahamu kuifanya teknolojia hii kuwa rahisi kuitumia. Kutokana na uzoefu wetu, tunaweza kuandaa na kuratibu shughuli za mikutano kwa njia ya video katika mji wowote duniani. Pia tuna uwezo wa kuunganisha mifumo/maeneo ya mikutano video zaidi ya mawili kwa wakati mmoja. Aidha, tunaweza kuunganisha mifumo ya video iliyo katika IP na ile ya ISDN.  

Elimu ya masafa na mafunzo kwa njia ya mtandao ni mtindo mpya wa elimu duniani. Kutokana na mahitaji ya kikazi, mahitaji ya kukaa na familia na majukumu mengine huwakwamisha watu wengi kusafiri kwenda kusoma darasani. Teknolojia imewasaidia watu kusoma popote walipo, wakati wowote.

Usimamizi wa mitihani ya mtandaoni haipaswi kuwa tatizo tena kwani TaGLA inatoa huduma ya usimamizi wa mitihani kwa wanaofanya mitihani ya aina hii. Sisi ni kituo cha mitihani cha kuaminika kimataifa, na ni wasimamizi mahiri wa mitihani.

Je, unatukio lolote litakalofanyika Tanzania? Kwa nini wewe usiendelee kushughulikia mambo mengine muhimu na ukatuachia kuratibu tukio hilo? TaGLA wana uzoefu mkubwa wa kuratibu matukio na shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa.